Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salamu za pongezi kwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
nchini Kenya (FKF), Nick Mwendwa kwa kuchaguliwa kuliongoza shirikisho
hilo.
Katika salamu hizo, Malinzi amempongeza Mwendwa kwa nafasi hiyo
aliyopewa kuliongoza soka la nchini Kenya, na kuahidi TFF itaendelea
kushirikiana nae katika maendeleo ya mpira wa miguu kwa ukanda huu wa
Afrika Mashariki.
Nick Mwendwa alishinda nafasi hiyo jana katika uchaguzi uliofanyika
jijini Nairobi kwa kupata alama 50 kati ya 77 za wapiga kura wote na
kupata nafasi hiyo iliyokua inashikiliwa na Samwel Nyamweya aliyemaliza
muda wake.

No comments:
Post a Comment