Saturday, June 17, 2017

Kipindi cha Amplifaya ya Clouds Fm cha futurisha

Kipindi cha #Amplifaya cha Clouds Fm mtangazaji Millard Ayo na Meena Ally waliandaa Iftar maeneo ya Mikocheni jengo la MayFair Plaza (Terrace lounge) na kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kushiriki na dhumuni ni kuchangisha kiasi cha pesa ambacho kitaweza kuwasaidia watoto yatima.

Waziri Makamba- 61% ya Tz hatarini kuwa jangwa

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira January Makamba (Mb) alieleza kuwa nchi yetu inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na hali ya kuenea kwa jangwa na ukame na kwamba takwimu zinaonyesha kuwa takribani asilimia sitini na moja (61%) ya eneo la nchi liko katika hatari ya kugeuka jangwa.

Tuesday, November 29, 2016

Madai ya Donald Trump yatupwa nje

White house (Ikulu) imesema hakuna ushahidi wowote wa kuashiria kwamba kulikuwa na wizi wa kura katika uchaguzi mkuu wa Marekani uliofanyika tarehe 8, Novemba mwaka huu.