Friday, February 12, 2016

Mwanamitindo wa Tanzania 'Herieth Paul' apata deal lingine Marekani.

Mtanzania anayefanya vizuri kwenye modeling jiji la New York, Marekani 'Herieth Paul', siku ya jana ameingia mkataba na kampuni kubwa ya makeup 'Maybelline' ya nchini humo, Mbali na kupata deal hili Herieth bado anafanya kazi na 'Tom Ford'.
Herieth ni kati ya wanamitindo wachache sana kutoka Tanzania wanaofanya vizuri sana nje ya mipaka ya Bongo (Flaviana Matata, Millen Magesse, Miriam Odemba) na kuzidi kuipeperusha ardhi yenye amani na upendo.



"Mkataba wangu na kampuni ya 'Maybelline' umeanza leo ila tulikuwa tuna negotiate for a month now but today everything is finalized na hauna end time, ni mkataba unao deal na mambo ya Makeup ambao nina represent all the dark skin girls around the world!.
Ingawa mkataba wangu hauniruhusu kufanya kazi sehemu ingine ila bado nafanya kazi na Tom Ford and also sisi ni marafiki wazuri sana."@heriethpaul

CMG: Je unaweza kuweka wazi kiasi gani cha fedha umeingiza?
HP: Aha siwezi kutoa kutoa information hiyo ila mkataba mzuri sana.
CMG: Mbali na fashion kuna kitu kingine unafanya?
HP: Yes! I'm going to school and also I'm a proud sponsor of kiwalani orphanage in Tanzania.
Kuwa sponsor ni kitu ambacho kina nipa furaha sana!! kuna wasichana watatu ambao hawana wazazi and also wana akili sana, me as a sponsor I take them to school and pay for their education! 2 of the girls are now heading to university!
CMG: Tangu ulivyoanza hadi sasa unaonaje soko?
HP: Fashion ina badilika kila siku!! Nashukuru mwenyezi mungu kwasababu dreams zangu zote zinaanza kutimia! One more dream/goal I'm hopping to accomplish by the end of 2016.

Credit: CMG

No comments:

Post a Comment