Wednesday, November 16, 2016

(Soma Hapa) Ommy Dimpoz kafunguka haya kwenye kipindi cha XXL



Baada ya jana Diamond Platnumz kufunguka yake kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm juu ya beef linaloendelea kati yake na mwanamuziki Ommy Dimpoz kuhusu vijembe vyao vya kupumuliwa na kununua viewers. Leo ilikuwa zamu ya Ommy Dimpoz kufunguka soma hapa.


“Nilipopost 'insta' kuhusu watu kununua 'views' YouTube, sikumtaja mtu, nilisema tu sasa hivi watu wanaweza kununua 'views', nafikiri sio kitu kizuri kwa sababu utakuwa unajidanganya unajitekenya huku unacheka mwenyewe, kwa sababu kuna jamaa alishawahi kunicheki kuhusu ishu hiyo, video yangu ya Wanjera ilikuwa na views laki tisa na laki nne ilikuwa imekaa mwaka mzima, akaniambia naweza kununua views nikamwambia kivipi, akaniambia nimtumie link baada ya masaa matano ikawa na views.
Baada ya kupost 'insta' kuwa kuna wasanii wananunua 'views' YouTube, nilikutana na meneja wa Diamond, Sallam akaniambia hakuna kitu ulichoniudhi kama kuongelea suala la views, nkamwambia kivipi akasema lazima utakuwa unamzungumzia Diamond, sijiamini, mara kwenye mtandao wakaanza kusema nina wivu.
Ukweli sikutaka kuongea kitu chochote, hata kwenye interview zangu sikutaka kuzungumzia 'ugomvi' wangu na Diamond, kwa sababu nilikuwa nikiamini ni upepo mbaya tu utapita, na mambo mengine yanaweza kuendelea mkapatana, mbona kuna watu wanagombana na Baba zao sembuse sisi, lakini vyanzo zilikuwa ni vingi sana, ushikaji wangu mimi na Diamond haujaanza leo, tangu naimba Top Band, hajatoa hata Nenda Kamwambie, alishawahi kuniambia watu wanataka nigombane naye ili asinipeleke kwa mganga wake, nikamwambia asiwajali hao wanaosema hivyo afanye kazi yake na isiharibu ushkaji wetu, lakini niwaka naona kadri siku zilivyokuwa zinakwenda mwenzangu alikuwa kama ananikwepa, kuna kipindi nilikuwa siwezi kufanya kitu chochote bila kumwambia yeye, wakati natoa Tupogo nilimsikilizisha akaniambia iko poa, nkamwambia nataka nmlete King Maluu aje kupiga saxophone kwenye hii nyimbo, cha kushangaza baada ya wiki nimepita zangu studio kwa Mackochalli namkuta Diamond na King Maluu anapiga saxophone kwenye wimbo wa Number One, alishtuka sana." 

Bdozen: Je tangu muwe marafiki na Diamond vitu gani uliwahi kuvichangia kwake…?
Ommy Dimpoz: Mimi sijawahi kusema sehemu yyt ila hili ndio mara yangu ya kwanza nalisema Ngoma ya nasema nawe ya diamond niuandishi wangu ila sijawahi ata siku moja kusema nimeandika mimi

No comments:

Post a Comment