Baada ya kuenea kwa maneno mengi juu ya msanii chipukizi kuondoka katika lebo ya 'The Industry Music' Seline amefunguka haya kupitia redio Choice FM kwenye kipindi cha Mji Wa Burudani.
"Mimi nilikuwa natafuta producer wa muziki nikaelekezwa kwa @Nahreel nikalipa na baada ya kulipa wakaniambia niwe chini yao nilikubali wanisimamie kazi zangu lakini kila nikiwauliza kazi zangu zitaanza kutoka lini walikuwa wakali.
@NavyKenzo wanavyosema wamenitoa kwenye uongozi wao kutokana na utovu wa nidhamu siyo kweli miezi 3 iliyopita ndio nilitoka chini ya @NavyKenzo na kabla sijatoka nilipeleka mkataba wangu kwa mwanasheria,Mwanasheria wangu aliniambia mkataba wangu hautanidhuru nikitoka chini yao na ndio maana haikuwa ngumu kwangu kutoka.
Wasanii ambao bado wapo chini ya @NavyKenzo walini unfollow baada ya kutoka chini ya 'NavyKenzo'." @Seline_Tz "

No comments:
Post a Comment