Friday, September 9, 2016

Kwa hili mabinti wengi wenye ndevu watajitokeza

Mwanamitindo mwenye ndevu za urefu wa nchi sita ametambuliwa na Guinness World Record kuwa mwanamke mwenye umri mdogo zaidi duniani kuwa ndevu zilizokomaa kabisa.

 
Harnaam Kaur, 24, ambaye ni mwanamke mtetezi wa kutambuliwa na kukubalika kwa hali ya mwili wa mwanadamu ulivyo bila ubaguzi anatoka Slough, Berkshire nchini Uingereza.
Amesema ni heshima kubwa kwake kutambuliwa.

Ameeleza ndevu hizo ndefu kama sehemu ya juhudi zake za kukabiliana na watu wengi waliomkejeli kutokana na muonekano wake.
Wengine waliotambuliwa kwenye rekodi za karibuni zaidi ni paka mrefu zaidi anayefugwa kama mnyama kipenzi pamoja na Ilama anayeruka juu zaidi.

No comments:

Post a Comment