Sunday, April 17, 2016

(Tazama Picha) Vyoo bora Duniani...je choo chako kipo...!!!

Tukisema vyoo ni muhimu sana kwenye jamii haijalishi kiwe katika mazingira gani ila tu kiwe katika hali usafi na salama kwa binadamu yoyote kutumia anapojisikia haja.


Kampuni moja ya usafiri 'Lonely Planet' iumeorodhesha vyoo vya kila aina ambavyo bila shaka vina uwezo wa kuwaacha wasafiri vinywa wazi au kuwa na kumbukumbu za kusalia nazo daima.
Hivi ni baadhi ya vyoo vilivyo kwenye mwongozo huo.













Vyoo hivi vinapatikana Chott, Tunisia katika ziwa la maji ya chumvi lililokauka. Hapa ndipo video ya nyumba ya Luke Skywalker katika filamu ya Star Wars ilichukuliwa.













Vyoo hivi katika eneo la Bahia, Brazil vimo katika kituo cha kutunza kasa













Choo hiki ambacho kinapatikana eneo lenye mandhari ya kupendeza kinapatikana Uswizi. Hapa ni mita 2,7000 katika milima ya Alps













Choo hiki katika duka la Standard Grill katika mtaa maarufu wa kufungia nyama New York kimeelezwa na wengi kama choo kinachokanganya ubongo.













Vyoo hivi vijulikanavyo kama Between The Waters vinapatikana Emscherkunst nchini Ujerumani.

No comments:

Post a Comment