Wanasayansi nchini
Uingereza wamepewa idhini na idara inayohusika na masuala ya uzazi ya
kufanyia viinitete vya binadamu mabadiliko ya kijenetiki.
Wanasayansi hao watafanya utafiti huo katika taasisi ya Francis mjini London.
Utafiti huo una lengo la kutoa uelewa kamili kuhusu siku za kwanza kwanza katika maisha ya binadamu.
Utaanza
siku saba za kwanza baada ya kukutana kwa chembe chembe za mme na mke
na kuonyesha kile ambacho husababisha mimba kutoka.
Mwaka uliopita
wanasayansi nchini China walitangaza kuwa walifanyia mabadiliko ya
kijenetiki viini tete vya binadamu kurekebisha hali ambayo husababisha
tatizo la damu.
Hatua hiyo imezua maoni tofauti huku baadhi
wakisema kuwa kuifayika mabadiliko DNA ni hatua ambayo imeenda mbali
zaidi na huenda ikasababisha kuzaliwa watoto waliotengezezwa.

No comments:
Post a Comment