Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa
Selestine leo amefungua kozi ya ngazi ya juu ya ukocha kwa wanawake
(High Level Coaching Course) iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na
FIFA.
Akiongea na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo,
Mwesigwa amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia mafunzo hayo na
kuitumia vyema fursa hiyo adimu waliyoipata.
Mwesigwa amewataka washiriki kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano,
inawasaidia na kwenda kuwa walimu wa mpira wa miguu kwa wanawake, na
kuongeza mwamko kwa wanawake wengi kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.
Aidha Mwesigwa, amewataka washiriki wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo
ya mkufunzi, nidhamu ya ndani na nje ya uwanja kwani imekua ni bahati
nzuri kwao kupata nafasi ya kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.
Naye mkufunzi wa kozi hiyo anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni
amesema atatumia uwezo wake wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo
wanajifunza na kuelewa vizuri mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu
wazuri watakapokwenda kuanza kufundisha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake ya TFF, Amina Karuma
ameishukuru TFF kwa kuendesha kozi hiyo na kusema kupatikana waalimu
wengi wa kike kutaongeza mwamko wa wanawake kuucheza mpira wa miguu.
Jumla ya washiriki 25 wanashiriki kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali
nchini ambao ni Fatuma Omary, Esther Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie
Charles, Pendo John, Berlina Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth
Sokoni, Sophia Mkumba, Marry Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.
Wengine ni Veneranda Mbano, Mariam Aziz, Hilda Masanche, Chichi
Mwidege, Sophia Edward, Asha Rashid, Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu
Muharami, Tatu Malogo, Komba Alfred, Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na
Ingfridy Kimaro.
No comments:
Post a Comment