Wednesday, January 27, 2016

Mambo mengine yameibuka kwenye gari la Wema Sepetu

Kipindi cha #xxl @cloudsfm kulikuwa na U- Head ya Soudy Brown na kayanasa mengine juu ya gari la Wema Sepetu aina ya Range Rover.


Amesema kulikuwa na stori kwamba kuna watu walikamata gari hiyo ikiwa haina baadhi ya nyaraka zake, mambo yakaenda baadae jamaa wakalikamata gari hilo..
Soudy akamcheki Martin Kadinda, jibu lake ni kwamba na yeye aliisikia story ya namna hiyo lakini hakuwa anajua kinachoendelea.
Martin amesema alimtafuta Wema, akaenda nyumbani kwake na kukuta gari hilo lipo, alipomuuliza Wema kama kuna ukweli wowote Wema hakumjibu zaiidi ya kumwambia hakuna sababu ya kuuliza gari wakati analiona lipo kwake halijakamatwa.
Hayo ndio ya Soudy Brown kwa leo, U Heard yote one to one na Martin Kadinda na stori yote ya gari sauti zao zipo kwa millardayo.com.


No comments:

Post a Comment