Wabunge wa
Uingereza wamekuwa na mjadala kuhusu kupigwa marufuku au la kwa
anayewania nafasi ya kupeperusha bendera ya chama cha republican katika
kinyang'anyiro cha urais wa Marekani, Donald Trump kuingia nchini
Uingereza.
Mjadala huo uliochukua muda wa saa tatu umekuja baada
ya karibu nusu milioni ya watu nchini Uingereza kuunga mkono hatua ya
kumzuia Trump kuingia Uingereza. baada ya Trump kusema kuwa Waislamu
wote wazuiwe kuingia marekani ikiwa ni njia ya kupambana na vitendo vya
kigaidi
Wabunge hata hivyo hawakuonyesha shauku kubwa ya kumfungia
milango Trump ili asiingie Uingereza kwani hakuna kura yeyote
iliyopigwa mwishoni mwa mjadala
Mmoja wa wabunge wa Uingereza
ambaye ni muislamu amesema kauli za Trump ni sumu, huku msemaji wa idara
ya mambo ya ndani Jack Dromey akisema kuwa Trump azuiwe kuingia
Uingereza.
Wakati huo huo Trump ameendelea na kampeni zake, akizungumza
katika chuo cha Liberty, chuo binafsi cha kikristo kilicho Lynchburg,
Virginia amewaambia wanafunzi wa kikristo kuwa wanapaswa kuungana
kuilinda dini yao.
''Tunapaswa kuilinda kwa kuwa kuna mambo
yanafanyika, mambo mabaya sana, sijui ni nini lakini hatuungani
labda.dini nyingine wanaungana kuzuia, hapa tunayo...ukitazama nchi hii,
asilimia 70 mpaka 75 ni wakristo, watu wengine wanasema hata zaidi ya
hiyo, inadhihirisha nguvu tuliyonayo, tunapaswa kuungana'' alieleza
Trump katika kampeni yake.

No comments:
Post a Comment