Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
amemteua makamu mpya wa Rais Emmerson Mnangagwa dalili kwamba huyo ndiye
Mugabe anampendekeza kumrithi.
Bwana Mnangagwa anachukua wadhifa huo kutoka kwa Bi Joyce Mujuru
ambaye Mugabe alimfuta kazi baada ya kumtuhumu kupanga njama ya kumuua.
Kwa jina la mzaha Mnangagwa anajulikana kama ‘Mamba’ mmoja wa watu wenye msimamo mkali wa chama.
Mugabe,mwenye umri wa miaka 90, alifanyia mabadiliko baraza lake la
mawaziri mnamo siku ya Jumanne huku akiendelea kung’ang’ania mamlaka.
Alichaguliwa kwa mara nyingine kama kiongozi wa chama tawala Zanu-PF
katika kongamano lake mwishoni mwa wiki wakati mkewe mwenye umri wa
miaka 49, Grace akiteuliwa kuongza tawi la wanawake wanachama wa chama
hicho.
Katika kauli yake ya kwanza tangu kupandishwa cheo, Bwana Mnangagwa
alionekana kuunga mkono mabadiliko yaliyofanywa katika chama hicho.
Bi Mujuru mwenye umri wa miaka 59, alionekana kama tisho kubwa kwa
bwana Mnangagwa katika ushindani wa uongozi wa chama hicho wakati Mugabe
atastaafu au kufariki.
Vyombo vya habari vya serikali kwa ushirikiano na Bi Grace Mugabe vimekuwa vikiendesha kampeini ya kumchafulia jina Bi Mugabe.
Hata hiuvyo amekanusha madai hayo akisema hakuna hata ushahidi mmoja
umetolewa dhidi yake kuthibitisha madai hayo kuwa alipanga njama ya
kumuua Mugabe ili amrithi kama kiongozi wa chama.
No comments:
Post a Comment