Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo, jimboni humo.
Mbunge wa Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika
uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo
wa kuiongoza Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo
endelevu wanayotaka Watanzania.
Amesema, yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine
watakaoona kuwa wanafaa kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila
atakayejitokeza itabidi kazi zake zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka
hafai.
Nyalandu ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa
Michezo wa Ilongelo jimbo la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia
kwenye kinyang’anyiro akiwa kifua mbele kutokana na kuamini kwamba
amekwishafanyakazi zilizotukuka.
“Kazi zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni
nzuri, hivyo yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa
kazi zetu kwa moto”, alisema Nyalandu
Itakapofika siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na
wana Singida Mashariki, na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania,
kwenda Dodoma kuchukua fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa
tiketi ya CCM”, alisema.
No comments:
Post a Comment