Monday, November 3, 2014

PENZI LA WEMA SEPETU NA DIAMOND PLATNUMZ LIMEOTA MBAWA!

Sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’. 
Safari hii ndiyo basi tena! Pamoja na kujishaua mbele ya kamera za wanahabari na simu za kuteleza (smart phones) kisha kutupia kwenye mitandao ya kijamii wakizuga wapo pamoja, habari ya mjini inadai kwamba, sexy lady wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ amemmwaga staa wa Ngoma ya Mdogomdogo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni rafiki mkubwa wa wapenzi hao, ishu ya kumwagana ilikuwepo muda mrefu lakini kinachoendelea ni kuwazuga mashabiki wao ili wasishuke kisanaa. 
SAFARI YA CHINA
Chanzo hicho kilifunguka kwamba, siku chache zilizopita Wema au Madam kama anavyopenda kuitwa, alimwambia Diamond kuwa anakwenda China kuchukua mzigo bila kumwambia ni mzigo gani na kwamba huko aliambatana na wanaume wanne, wawili wakiwa ni Martin Kadinda na Petit Man. 
KAMA MBWAI, IWE MBWAI 
Ilidaiwa kwamba wanaume wengine wawili wapo kwenye mabano, jambo ambalo Diamond au Dangote kama anavyopenda kujiita, hakuliafiki suala hilo lakini Madam akasema liwalo na liwe yaani kama ‘mbwai iwe mbwai’ hivyo akampuuza na kwenda zake China! 
AHADI HEWA? UBAHILI WAMPONZA DIAMOND
Chanzo hicho kiliendelea kumwaga ‘ubuyu’ kwamba, tabia ya Diamond ya ubahili, nayo imechangia kwa Wema kukaa pembeni kwani jamaa huyo siyo mkataji wa mkwanja kama ilivyokuwa kwa yule kigogo wa Wema, Clement.

No comments:

Post a Comment