Staa wa Nigeria Wizkid amekuwepo Afrika Mashariki kwa takribani wiki moja. Alianzia jijini Nairobi Kenya ambapo Jumapili iliyopita alitumbuiza kwenye viwanja vya The Carnivore, na baadae kuelekea jijini Kampala Uganda ambako alitumbuiza kwenye Party ya Guiness na kisha akarudi tena Kenya ambako imefahamika alirudi kushoot video.
Victoria Kimani (kushoto) Wizkid (Kulia) Staa huyo wa ‘If I Show You My Money’ ameshoot video nchini Kenya na director Mkenya Enos Olik ambaye amewahi kufanya video za wasanii wa Bongo kama Weusi (Gere), Vanessa Mdee (Come Over) na video mpya ya Shaa (Njoo).




No comments:
Post a Comment