Rais wa Brazil Dilma Rousseff amechaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo.
Matokeo
rasmi ya uchaguzi huo yanaonesha Bi Rousseff ameshinda kwa Asilimia
tatu ya kura katika uchaguzi uliojaa ushindani mkali dhidi ya mpinzani
wake, mwanasiasa mwenye mrengo wa kati kulia Aecio Neves, ambaye tayari
amekubali kushindwa.
Akiwashukuru wapiga kura wake, Dilma Rousseff amesema anataka kuwa Rais bora zaidi na kipaumbele kikuu katika awamu yake ya pili ya uongozi itakuwa ni kufanya mageuzi ya kisiasa.
Mwandishi wa BBC nchini Brazil amesema wapiga kura wameamua kuendelea kumchagua, Bi Rousseff wakiunga mkono mfumo na chama ambacho kimeukuza uchumi wa nchi hiyo na mipango mingi kuhusiana na ustawi wa jamii hiyo, ambavyo vimewatoa katika umasikini uliokithiri.
Hata hivyo, mwaka uliopita uongozi wake alikumbana na upinzani mkali kuhusiana na kashfa ya rushwa, juu ya matumizi makubwa ya fedha yaliyofanywa wakati wa maandalizi ya kombe la dunia na huduma mbovu.
Bi Rousseff ambaye anawakilisha chama cha wafanyakazi ambacho kimekuwa madarakani kwa miaka 12, amepata asilimia 51,48 ya kura zote zilizopigwa huku mpinzani wake Aecio Neves, kutoka chama cha Social Democratic Party akipata asilimia 48,52 ya kura, na kukubali matokeo.
Kinyanganyiro hicho kupata nafasi hiyo ya Urais, kinaelezwa kuwa kikali zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadha nchini Brazil.

No comments:
Post a Comment