Kwanza nianze kwa kukili kua maisha ni magumu sana nadhani kila mtu anajua, na katika mahusiano ya mapenzi kati ya mwanaume na mwanamke lazima kunakua na tofauti ya kipato na mara nyingi wanaume wanakua na hali nzuri kwenye kipato kuliko mwanamke.
Nieleweke vizuri kua si wanawake wote wanakipato duni la hasha, ningependa kuwashauri wale wenye wapenzi wa kike mambo haya yafuatayo:1 Ujue tofauti ya kuchunwa na kuhudumia unapokua na mpenzi ujue ni jukumu lako kumpendezesha anapopendeza watu watajua we ndio kidume uliemwezesha. 2 .Sio mpaka akuombe ndio umpe. jaribu kumfaam hali ya maisha na kipato chake ujue kukisia cha kumpa kwa matumizi yake. 3.Usiulize ya nini,ikitokea mpz amekuomba hela usiulize ya nn ye ni mtu mzima awezi kukuomba hela akaenda kuchambia. 4. Kutumia pesa nyingi sehemu ya starehe. Kuna watu wanaenda mpaka hotel ya nyota 5 kustarehe akitumia zaidi ya laki tano na cha ajabu baada ya kutoka hotel anamwacha mpz wake 10,000 ya nauli. Huu ni ujinga bora ungeenda ata lodge ya nafuu ye ukamwacha na mkwanja wa kutosha. 5. Tenga ata 10% ya mshahara mpe yeye aangalie kama kuna kitu cha kurekebisha arekebishe. APA ni kwa wale Wanaume wanaowazidi kipato wanawake wao sio wanawake wenye vipato vizuri. Tusiwe wataalamu wakutafuta Gspot wakati ukiombwa ata 1,000 unanuna mapenzi ni pamoja na kupunguzia makali ya maisha. Yeyote mwenye chochote anaweza kuongezea apo.

No comments:
Post a Comment