Masikini Akipata Matako Hulia
Mbwata, bwana mdogo Diamond mtoto wa Tandale ambae wakati Wema Sepetu
anakuwa miss yeye alikuwa anauza mitumba kule Tandale kapata pesa sasa
naona makalio yake yanalia Mbwata.
Kama unampenda sana Diamond usipanic endelea kusoma utanielewa tu
Diamond amewakera mashabiki ndio maana yamemkuta yale yaliomkuta pale
Leaders. Kijana Diamond alikuwa moja kati ya watu masikini sana nchini,
alikuwa ANALALA kwenye mazingira magumu ila leo amediriki kusema kuwa
MBEYA HAKUNA HOTELI YENYE HADHI YAKE, hahahaa inachekesha sana. Anasahau
kuwa umaarufu wake umekuja kwasababu mashabiki WALIAMUA kumkubali.
Wema Sepetu wakati ana make headlines akiwa Miss Tanzania hakuwa
anatambua kuwa pale mitaa ya Tandale kuna kijana anaitwa Nassibu anauza
mitumba, na ninaamini hata kama angeonana na Diaomnd kipindi kile HAKIKA
asingemuangalia mara mbili. Ila dogo leo kapata hela anaanza kuleta
dharau kwa mashabiki. Dogo ana kauli chafu sana, anapenda kujikweza.
Ukitaka ufanikiwe na ufaidi kuwa msanii bongo hakikisha UNAWAFURAHISHA
mashabiki wako mdogo wangu. Waache watu wakusifie wewe. Kitu ambacho
hujui ni kwamba hapa bongo kulikwa na wasanii wakubwa kama akina Mr.
Nice lakini walilewa sifa na sasa wanaishia kucheza pool pale sinza
ambiance na kutia huruma. Usipoangalia wewe na kaka yako Nice mtaakaa
kijiwe kimoja na kusema ZAMANI NILIKUWA MAARUFU.
Diamond
umekuwa na tabia ya kusema wewe ni maarufu na kukataa mara kadhaa (HATA
UKIOMBWA) kufanya show sehemu mbali mbali, unajiona ni msanii wa kufanya
SHOO ZA MILL 30, kuna cases kadhaa za wewe kuwatolea nje mashabiki
kufanya shoo eti kwa madai unataka hela nyingi. Unasahau watanzania hawa
hawa ndio waliokupigia kura ukapata hizo tuzo na kuwa nominated hata
kwenye hizo BET, lakini naona sasa UMEUCHOKA umaarufu wako na uko tayari
kuupoteza kwa upuuzi tu usio wa maana.
Kuna mambo mengi sana
unakosea kama binadamu ila kuna mengi unayafanya makusudi kwasababu wewe
ni LIMBUKENI, kwa mfano suala la kutoka na mabinti kadhaa wa kadhaa
kwako umeona kama ni ufahari hivi, kumbe wenzako wanakuona zuzu tu cuz
huwezi kuwamaliza mabinti wote duniani. Na kwasababu hiyo ndio maana
wanaume wenye akili WAMEMUHONGA WEMA GARI wakasingizia kuwa ni Kadinda
ndie alietoa, ukiacha dharau watu watakuheshimu.
Sijui
niendelee au niishie hapa?! Aah nikiishia hapa ntakuwa nimekuogopa.
Mdogo wangu wewe kimziki sio kwamba uko juu sanaaaa kuliko Alikiba,
Linex, Barnaba, Ben Paul au hata lady jaydee ni kwamba umepata promo
nyingi sana kiasi cha mashabiki KUAMUA kukukubali. Unashangaa watu pale
leaders waliamua kukuzomea ni kwasababu watanzania wamechoka na majivuno
yako na dharau. Sasa T.I anataka kufanya collabo na Ali Kiba ile
inaonyesha dhahiri kuwa wewe BADO. Anyways kama umemaindi poa ila hayo
ni maoni yangu kama SHABIKI na ungekuwa wewe ni chama cha siasa hakika
leo ningerudisha kadi yangu ya Uanachama mpaka pale utakapojirekebisha!
Usije ukakonda bure kwa makavu haya. La mwisho Gwanda zile zitakuletea
matatizo, inawezekana ulionywa hukusikia jaribu tena uone cha mtema
kuni. Next time hutaitwa Oysterbay watakuficha wenye nazo!
Source: Umbea mtupu

No comments:
Post a Comment