Rais mteule wa
Marekani 'Donald Trump' ametetea utaratibu wa mpito nchini humo na kusema
hakuna mzozo kinyume na inavyotangazwa kwenye vyombo vya habari.
Trump ameandika kwenye Twitter kwamba shughuli ya kuwachagua mawaziri
wake inaendelea na ni yeye pekee anawajua watu
watakaoteuliwa.
Mbunge wa zamani (Mike Rodgers) aliyekuwa akisimamia masuala ya Usalama wa taifa katika kundi la mpito amejiuzulu.
Kumekuwa na taarifa kwamba alisukumwa nje na shemejiye Bw Trump.
Taarifa katika vyombo vya habari zimedokeza kwamba kuna mzozo
mkali miongoni mwa maafisa wanaosimamia shughuli ya mpito upande wa Bw
Trump, ambao makao makuu yao yamo katika jumba la Trump Tower, New
York.
Meya wa zamani wa New York, Rudolph Giuliani, ambaye
anatarajiwa kupewa wadhifa mkuu, amesema shughuli ya mpito huwa ngumu na
ni kawaida kukumbwa na matatizo madogo hapa na pale.

No comments:
Post a Comment