Ni watu wachache walikuwa na fikra kuwa angeweza kuwania, lakini yeye alifanya hivyo. Walifikiri hangepata umaarufu lakini akafanya hivyo.
Wakasema hangeweza kushinda mchujo wowote lakini akafanya hivyo. Wakasema hangeweza kushinda uteuzi wa Republican lakini akafanya hivyo.
Majimbo yaliyokuwa ngome ya Democratic yote yalimpigia kura Trump yakiwemo Ohio, Florida na North Carolina.
Watu wazungu walio na ajira hasa wale wasio na masomo ya chuo kikuu wanake kwa wamaume walikihama chama kwa wingi.
Licha wa majimbo kama Virginia na Colorado kumchagua Clinton, jimbo la Wisconsin lilimwendea Trump na kusababisha matumaini ya Clinton kudidimia.
Trump alimdhalilisha John McCain. Akaanza ugomvi na mtangazaji wa kituo cha Fox News Megyn Kelly.
Alipambana na pingamizi ndani ya chama chake na kushinda zote.
Trump alijenga himaya yake kutoka wa washindani wake kaiam mchujo. Wengie kama Marco Rubio, Ted Cruz, Chris Christie na Ben Carson baadaye walisalimu amri.
Ni dalili ambayo wanasiasa wengine waliiona kwa mbali, Bernie Sanders na Tedd Cruz kwa mfano.
Lakini hata hivyo hakuna mtu aliyeilewa kama Trump mweyewe na ndivyo ikampeleka ikulu ya White House.

No comments:
Post a Comment