Mwanamuziki wa Uingereza ameahirisha tamasha lake la muziki visiwa vya Caribbean baada ya mbwa wake kuugua.
Joss Stones alisema mbwa huyo kwa jina Missy ni kama mtoto kwake.
Aliandika
kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba aliahirisha tamasha ya Jumamosi
kisiwa cha Barbados na Jumanne kisiwa cha Trinidad baada ya mbwa wake
kuanza kuvuja damu.
“Najua linaonekana kama jambo la kushangaza lakini kwangu mbwa huyu ni kila kitu,” aliongeza.
“Nawaahidi nitarejea, lakini kwa sasa Missy yuko mbele ya mambo mengine yote,” aliandika.
Amesema anatumai kufanya onesho nchini Venezuela tarehe 21 Aprili mambo yakiwa sawa. Stone tayari ameandaa maonesho India, Nepal, Panama
na Costa Rica kama sehemu ya safari yake nchi mbalimbali duniani
kuvumisha albamu yake ya saba kwa jina Water For The Soul.

No comments:
Post a Comment