Wednesday, March 2, 2016

Mtoto wa Raila Odinga: atoa boko la 'Olduvai Gorge'

Kumekuwa na hali ndivyo sivyo kwa nchi zingine kufananisha Wachezaji, Wanamuziki na baadhi ya Vivutio vyetu kama wapo kwao, jambo hili linaleta mashaka kwa Watanzania why kila siku sisi, Binti wa Raila Odinga (Rosemary Odinga) nae katoa mpya baada ya kusema Olduvai Gorge ipo Kenya.

  • Mwanawe aliyekuwa waziri mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Rosemary, amekiri kuwa alikosea alipodai kuwa bonde la Olduvai Gorge liko Kenya ilhali liko Tanzania.
''Bonde la Oldupai ama Olduvai liko Tanzania, nimekubali kuwa nilikosea nilipokuwa nikihutubia mkutano wa viongozi wa vijana kutoka kote duniani nikiwa New York Marekani(International Young Leaders Assembly).
''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.
''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado.
''Nahisi kama ambaye nimewakosea ndugu zangu kutoka Tanzania''.
''Nia yangu ilikuwa ni kusema kuwa nilipokuwa mdogo nikienda shuleni nilifunzwa kuwa fuvu la mtu wa kale lilipatikana Olorgesaiile eneo la Kajiado.
               
Nisemeje ,,nawaombeni radhi Watanzania.
Olduvai Gorge iko salama wala haijanyakuliwa na kenya
'Katika ile hali ya undugu naomba kuwanyoshea mkono wa amani kwa sababu mwisho wa siku Afrika mashariki ndio kitovu cha ubinadamu'' alisema bi Odinga kupitia mtandao wake wa Instagram.

No comments:

Post a Comment