Mwanawe mwimbaji
maarufu marehemu Whitney Houston alifariki baada ya kuzama majini pamoja
na ulevi wa dawa za kulevya ,ripoti ya matibabu imebaini.
Marehemu
Bobbi Kristina aliyekuwa na umri wa miaka 22 alifariki katika hospitali
moja tarehe 26 mwezi Julai ,miezi sita baada ya kupatikana bila fahamu
katika choo cha kuoga.Jaji mmoja mjini Atlanta alitoa agizo siku ya Alhamisi la kuiweka wazi ripoti hiyo kufuatia ombi la vyombo vya habari.
Waliofanya uchunguzi huo wanasema kuwa walichunguza rekodi za matibabu za msichana huyo na stakhabadhi nyengine ili kubaini chanzo cha kifo cha mwanadada huyo wa Marekani.

No comments:
Post a Comment