Tuesday, January 19, 2016

Venus Williams ashindwa kufua dafu mbele ya Konta.

Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Marekani 'Venus Williams' ameshindwa kufua dafu mbele ya mchezaji kutoka Uingereza 'Johanna Konta' baada ya kushinda 6-4 6-2 dhidi ya Venus katika raundi ya pili ya shindano la tenisi la Australian Open mjini Melbourne.

Konta, 24, alipata ushindi kwa kutumia dakika 79 huku bingwa wa Grand Slam Williams, ambaye alikuwa amefungwa bendeji paja lake la kushoto, akionekana kutatizika.
“Droo ilipofanywa na nikaona nilikuwa nimepangwa kucheza na nani, niliomba tu niweze kudumu uwanjani zadi ya saa moja,” amesema Konta.
Konta, aliyefika hatua ya 16 bora katika US Open mwaka 2015, sasa atakutana na mshindi kati ya Carina Witthoeft na Saisai Zheng, katika raundi ya pili. Konta aliyeorodheshwa nambari 47 duniani, alikuwa akicheza mara ya kwanza katika Australian Open na ndiye mwanamke Mwingereza pekee aliyesalia katika droo ya mashindano ya mchezaji mmoja mmoja baada ya Heather Watson kushindwa Jumatatu.

No comments:

Post a Comment