Ligi kuu ya soka ya England inatarajiwa kuendelea tena wikendi hii kwa michezo kumi baada ya mapumziko kupisha Mechi za FA.
kesho
jumamosi jumla ya michezo nane itapigwa katika viwanja mbalimbali
ambapo mechi hizo ni Norwich city watawaalika Liverpool, Crystal Palace
watakuwa wenyeji wa Tottenham, Leicester dhidi ya Stoke,Man Utd watakuwa
nyumbani dhidi ya Southampton, Sunderland watachuana na Bournemouth,
Watford watakuwa wenyeji wa Newcastle, West Brom watawaalika Aston Villa
na Man City watakuwa wageni wa West Ham United.
Jumapili ligi
hiyo itaendelea tena kwa michezo miwili ambapo Everton watakuwa wenyeji
wa Swansea city na Arsenal watakuwa nyumbani Emirate dhidi ya Chelsea
(The blues).

No comments:
Post a Comment