Kanisa la urefu wa
mita 16 lililojengwa kwa kutumia vigae vya glasi linalofanana na viatu
vyenye visigino virefu vinavyopendwa sana na wanawake limejengwa huko
Taiwan kwa lengo la kuwavutia wanawake zaidi.
Picha iliopigwa juu ya kanisa hilo pia imeonyesha ukubwa wa kanisa hilo pamoja na uzuri wa eneo lililojengwa.
Jumba hilo la kuabudu linatarajiwa kufunguliwa tarehe 8 mwezi Februari tayari kwa mwaka mpya wa Uchina.
Kiatu hicho kimetengezwa na maafisa wa baraza la
miji kusini magharibi mwa pwani ,katika eneo moja la kitalii lenya
umaarufu mkubwa huko Taiwan.
Lakini Pan Tsuei-ping,msimamizi wa ujenzi huo,ameiambia BBC kwamba kanisa hilo halitatumika kwa huduma za ibada za kila siku bali hafla za harusi.
''Katika mipango yetu,tunataka kulifanya eneo hili kuwa la kuvutia kimapenzi,kila msichana angepanda kutafakari atakapokuwa bibi harusi alisema'', Pan aliiambia BBC.

No comments:
Post a Comment