Kama ulisikia kuhusu mauji ya Wanawake mbalimbali kwenye jiji la Dar
es salaam utakua ulitamani kujua wanaohusika manake stori zilikua
zinaripotiwa tu na taarifa zinazoambatana nazo ni kwamba uchunguzi
unaendelea.
Sasa mpaka sasa unaambiwa ni zaidi ya Wanawake 11 wameuawa Dar es
Salaam katika kipindi cha miaka miwili na kutupwa barabarani au mitaroni
huku miili yao ikiwa imefanyiwa vitendo vya unyama na udhalilishaji.
Kutokana na mauaji kuendelea, Polisi wamefanikiwa kuwakamata watu
wawili akiwemo ABOUBAKAR KASSANGA Mkazi wa Mwenge na EZEKIEL ASENEGALA
mkazi wa Tandika Dar es Salaam ambao wamekiri kuhusika na vitendo hivyo
ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA
amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao ambao pia wamekiri kuwauwa
wasichana wawili hivi karibuni waliotajwa kwa majina ya WANZE MAKONGORO
na JACKLIN MASSANJA wamesema wamekuwa wakiwalaghai wasichana kimapenzi
na badae kuwaua.
Katika hatua nyingine Kamishna KOVA ametoa tahadhari kwa wasichana
kuacha tabia ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa ghafla na watu
wasiowafahamu ambapo tukio la mauaji ya wasichana hao wawili lilitokea
Novemba 19 mwaka huu ambapo baadhi ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya
wasichana hao vimekutwa mahala wanapoishi watuhumiwa hao.
Kamishna KOVA amesema upelelezi bado unaendelea ili kuunasa mtandao mzima wa uhalifu huo.

No comments:
Post a Comment