Thursday, December 11, 2014

MISS TZ HAPPINESS WATIMANYWA AMEINGIA TOP 10 MISS WORLD 2014

Jana December 10. 2014 Watanzania walimpokea kwa shangwe mwakilishi wao kutoka kwenye mjengo wa BBAHotshots Afrika Kusini, Idris Sultan ambae ndie alitangazwa mshindi wa dola za kimarekani laki tatu siku kadhaa tu baada ya Diamond Platnumz kuing’arisha Bongo kwa kushinda tuzo 3 za Channel O.


Habari njema ingine ni mshiriki wetu kwenye Mashindano ya Miss World, Happiness Watimanywa ambae masaa machache yaliyopita imethibitika kwamba ameiwakilisha vizuri Tanzania na kuifanya iingie kwenye kumi bora za mashindano ya Miss World People’s Choice.
Happiness aliandika kwenye instagram “Tanzania Asanteni kwa support na uzalendo, tuendelee mpaka namba moja!!!!! #vote #PigaKura #DownloadTheApp #MissWorld2014”– @happinesswatimanywae.
Katika list hiyo, Happiness ameshika nafasi ya tisa katika kumi bora kama inavyoonekana hapa chini.
Happy Watimanywa iii
Happy Watimanywa

No comments:

Post a Comment