Serikali ya Tanzania imeyafungia
kwa miaka miwili mashindano ya Miss Tanzania baada ya waandalizi kudaiwa
kukiuka taratibu na kanuni.
Mashindano hayo yaliofunguliwa mwaka 1994 yamedaiwa kuwa na
upendeleo mbali na rushwa kulingana na malalamishi yaliotolewa na
wananchi pamoja na washiriki.
Kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini
Tanzania Basata , Godfrey Mngereza,kamati ya miss Tanzania ilikiuka
kanuni na taratibu zinazoongoza mashindano hayo.
Alisema bwana Mgereza:”Ni kweli kwamba tumeifungia Miss Tanzania
kwa miaka miwili, lakini haya si maazimio ya tathmini iliyofanyika
mapema mwezi huu, bali kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyofanyika na si
kimoja, ni uamuzi mgumu ambao umekuja kutokana na sababu maalumu,”
Imedaiwa kuwa mashindano yaliyofanyika Desemba 12, mwaka huu
hayakufikia uamuzi, bali vikao mbalimbali vilivyoendeshwa na wizara ya
Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Basata ndivyo
vilivyofikia hatua hiyo ili kutoa nafasi kwa waandaalizi kujipanga upya.
Baadhi ya maswala yaliobainika ni kwamba baadhi ya warembo
walidaiwa kutumiwa kingono.Vilevile hakuna utaratibu wa kuwasajili
warembo hao uliofuatwa kuanzia vitongojini hadi kufikia fainali.
Mngereza alisema baraza limegundua kuwa baadhi ya washiriki walichaguliwa kwa upendeleo bila ya kuwa na sifa zilizohitajika
No comments:
Post a Comment