Jeshi
nchini Pakistan linasema limewakamata watu 10 wanaoshukiwa kupanga na
kufanya shambulio dhidi ya msichana wa shule nchini humo Malala
Yusufzai.
Msemaji wa jeshi meja jenerali Asim Salim Bajwa amesema silaha iliotumika katika shambulio hilo imepatikana.
Amesema kundi hilo liliagizwa na mkuu wa kundi la Taliban, Mullah Fazlullah, kutekeleza shambulio hilo.
Malala Yousufzai alipigwa risasi mara tatu kwa karibu miaka miwili iliyopita na wanaume waliojihami kwa bunduki walipanda basi la shule alimokuwa Malala, katika wilaya ya Swat iliyopo kaskazini magharibi mwa Pakistan na wakamuita kwa jina.

No comments:
Post a Comment